• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 18, 2019

  RONALDO AFUNGA BAO LA 99 KIMATAIFA URENO YASHINDA 2-0

  Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Ureno bao la pili dakika ya 86 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Luxembourg kwenye mchezo wa Kundi B kufuzu Euro 2020 usiku wa jana Uwanja wa Josy Barthel mjini Luxembourg, hilo likiwa bao lake la 99 katika mechi za kimataifa. Bao la kwanza la Ureno lilifungwa na Bruno Fernandes dakika ya 39 na kwa ushindi huo mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 17 katika mchezo wa nane wakiendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Ukraine yenye pointi 20, hivyo wote kufuzu fainali zijazo za michuano hiyo 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AFUNGA BAO LA 99 KIMATAIFA URENO YASHINDA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top