Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BEKI wa Ruvu Shooting, George Michael aliyemkaba koo mshambuliaji wa Yanga SC, Amisi Tambwe shauri lake litafutiwa siku maalum ya kusikilizwa.
Hatua hiyo inafuatia beki huyo timu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kutohudhuria kikao jana kwa sababu alikuwa ana udhuru.
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kesi ya mchezaji huyo itasikilizwa siku nyingine, lakini imewafungia Aggrey Morris na Juma Nyosso kwa ‘mchezo mbaya’.
Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya 11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa, kudhalilisha utu wa mtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira wa miguu.
Naye Morris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa hatiani kwa kumpiga mshambuliaji
Emmanuel Okwi wakati timu hizo zilipopambana kwenye mechi ya ligi iliyochezwa Januari 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kabla ya kusoma uamuzi, Wakili Msemwa alisema mlalamikiwa Morris alikiri kugongana na
Okwi, kwa maelezo kuwa aliingia kwenye 'reli' ndiyo ukatokea mgongano huo.
Kamati baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Simba, ripoti za Brain CT scan kutoka Besta Diagnostic Centre na nyingine kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), taarifa za madaktari zilionyesha Okwi aligongwa kichwani akiwa anacheza mpira na kuzimia kwa dakika tano, pia mkanda wa video uliowasilishwa na TFF imeona kulikuwa na kugongana kati ya wachezaji hao.
Hivyo, Kamati ikamtia hatiani Morris kwa kutumia Ibara ya 48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012 kwa kumfungia mechi hizo tatu na kumpa onyo kali.
Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu ya Friends Rangers kupinga refa
kuchezesha mechi yao dhidi ya Majimaji kwenye mvua kubwa, kutoa maamuzi yasiyo
halali na kutokuwepo na ukweli kwenye ripoti ya Kamishna yakasikilizwe na Bodi ya Ligi kwa vile si masuala ya kinidhamu.
Wachezaji watatu wa Friends Rangers; Mahmoud Othman, Khalid Twahil na John Alexander wamefungia miezi sita na faini ya sh. 500,000 kila mmoja kwa kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Majimaji.
Licha ya wachezaji hao kuitikia mwito wa Kamati, wachezaji hao walizuiwa na viongozi wa
kuingia ukumbini wakati malalamiko dhidi yao yalipoanza kusikilizwa. Hatua hiyo iliifanya Kamati ifanye uamuzi baada ya kuusikiliza upande wa walalamikaji pekee.
Kamati hiyo, pia imemfungia miezi sita na kumpiga faini ya sh. 200,000 Meneja Vifaa
(Kit Manager) wa timu ya Polisi Mara, Clement Kajeri kwa kuhamamisha vurugu na
kuwapiga waamuzi kwenye mechi dhidi ya Mwadui iliyochezwa Uwanja wa Karume
mjini Musoma. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.

George Michael kulia hakutokea katika kikao cha Kamati ya Nidhamu TFF |

0 comments:
Post a Comment