// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YAYA TOURE ASEMA MAN CITY KUTETEA UBINGWA SI KAZI RAHISI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YAYA TOURE ASEMA MAN CITY KUTETEA UBINGWA SI KAZI RAHISI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 09, 2015

    YAYA TOURE ASEMA MAN CITY KUTETEA UBINGWA SI KAZI RAHISI

    NAHODHA wa Ivory Coast, Yaya Toure amesema kwamba klabu yake, Manchester City inatakiwa kushinda mechi zote zilizobaki ikiwa inataka kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
    Akizungumza baada ya kuwaongoza Tembo kushinda taji la Kombe la Mataifa ya Afrika, Toure ambaye alikandiwa kwa kucheza chini ya kiwango kwenye baadhi ya mechi za AFCON alisema yuko tayari kurudi kazini Man City.
    Lakini klabu yake ikiwa inazidiwa pointi saba na vinara Chelsea, nyota huyo wa Ivory Coast amesema hiyo si kazi rahisi.
    Yaya Toure, pictured after winning the Africa Cup of Nations, insists Manchester City can win the league
    Yaya Toure akipokea Kombe la Afrika jana mjini Bata, Equatorial Guinea baada ya kuiongoza Ivory Coast kushinda kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120

    "Kwa kujiamini kwangu, najua soka si kuhusu mchezo mmoja, au miwili hususan katika Ligi Kuu ya England,"amesema.
    "Tuna mechi 38 na ikiwa tunataka kushinda (kutetea ubingwa) tunatakiwa kushinda mechi zote. "Nafahamu ni vigumu, lakini nafahamu natakiwa kurejea na kufanya kazi yangu tena,".
    Toure alifunga mkwaju wake wa penalti wakati matuta jana Ivory Coast ikiibwaga Ghana 9-8 na kutwaa Kombe- na sasa anarejea England kuisaiedia Man Citu viya ya kutetes taji baada ya kukosekana tangu mwezi uliopita.
    Na Manchester City haijashinda mechi hata moija tangu Mwanasoka huyo Bora wa Afrika aende kwenye AFCON.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE ASEMA MAN CITY KUTETEA UBINGWA SI KAZI RAHISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top