KLABU ya Real Madrid itaingia kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya mahasimu wa Jiji, Atletico Madrid bila ya wachezaji wake wawili tegemeo, James Rodriguez na Sergio Ramos walioumia usiku wa jana.
Kikosi cha Carlo Ancelotti kiliifunga Sevilla mabao 2-1 kuendelea kuongoza kwa pointi nne zaidi La Liga, na sasa wanaelekeza nguvu zao kwa wapinzani wao wa jiji la Madrid, wakiwakosa baadhi ya wachezaji muhimu.
James Rodriguez na Sergio Ramos wote walitolewa nje ndani ya dakika 25 Uwanja wa Bernabeu baada ya kuumia. Na taarifa imethibitisha Ramos ameumia nyama za paja, wakati maumivu ya Rodriguez ni makubwa, amevunjika mguu na atahitaji upasuaji.
Sergio Ramos (kulia) akiwa ameshika nyama za paja wakati anatoka jana
0 comments:
Post a Comment