// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NDANDA YASHINDWA KUFIKIA MALENGO YAKE RAUNDI KWANZA MEISHA IKIWA MKIANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NDANDA YASHINDWA KUFIKIA MALENGO YAKE RAUNDI KWANZA MEISHA IKIWA MKIANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, February 04, 2015

    NDANDA YASHINDWA KUFIKIA MALENGO YAKE RAUNDI KWANZA MEISHA IKIWA MKIANI

    Na Juma Mohammed, MTWARA
    TIMU pekee inayowakilisha mikoa ya kusini, Ndanda FC imemaliza raundi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara huku ikishindwa kufikia malengo iliyopanga
    Akizungumzia  mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo Afisa habari wa ndanda Idrisa Bandali amesema walipanga kumaliza mzunguko wa kwanza  wakiwa nafasi tatu za juu lakini malengo hayo yamefeli huku wakiambulia nafasi ya tatu mkiani
    ”Tumeshindwa kufikia malengo lakini kila mtu ameona tunavyocheza tunabadilika kila mchezo ligi ya mwaka huu ni ngumu sana ila bado tuna nafasi ya kufanya vizuri  kwani hata bingwa bado hajajulikana “ alisema Bandali.
    Kikosi cha Ndanda kimemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kikiwa mkiani

    Timu hiyo ambayo ilianza kwa mbwembwe baada ya kuanza ligi kwa kuwatandika goli nne Stand united wakiwa ugenini lakin baadae ilipoteza mvuto kwa mashabiki wake baada ya kushindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kujikuta ikiambulia pointi nne tu katika mechi nne za nyumbani
    Timu hiyo kwa sasa ipo nyumbani mtwara ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa nangwanda sijaona mjini hapa tayari kujiandaa  na raundi ya pili ambapo itafungua na Stand United katika mchezo utakaocheza hapahap Mtwara.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDANDA YASHINDWA KUFIKIA MALENGO YAKE RAUNDI KWANZA MEISHA IKIWA MKIANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top