KLABU ya Manchester City inaendelea kumfuatilia kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone kwa ajili ya kumchukua.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England, wameachwa pointi saba na vinara Chelsea baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Hull City.
Timu hiyo ya Manuel Pellegrini sasa ipo kwenye hatari ya kumaliza msimu bila taji baada ya kutolewa kwenye mashindano yote ya nyumbani katika hatua za mwanzoni. Mbali na mbio za ubingwa wa Ligi Kuu, zaidi Man City itajaribu bahati yake kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Diego Simeone yuko kwenye rada za Manchester City
Februari 24, mwaka huu, Manchester City itamenyana na Barcelona kwa mara ya pili mfululizo na kipigo kingine kwa Pellegrini kitaibua maswali juu ya mustakabali wa Mchile huyo.
Simeone aliiongoza Atletico kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Hispania,maarufu La Liga pamoja na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambako walifungwa na mahasimu wao, Real.
Lakini Simeone akalipa kisasi cha kufungwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa, kwa kuitandika 4-0 timu ya Carlo Ancelotti Jumamosi.
Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 44 ndiye anaonekana mtu aliye tayari zaidi kumrithi Pellegrini. Wote Ancelotti na koca Bayern Munich, Pep Guardiola hawategemewi kuondoka katika klabu zao, wakati Jurgen Klopp amekuwa na msimu mbaya
0 comments:
Post a Comment