// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KOPUNOVIC: SIMBA SC NA COASTAL PATACHIMBIKA MKWAKWANI LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KOPUNOVIC: SIMBA SC NA COASTAL PATACHIMBIKA MKWAKWANI LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, February 07, 2015

    KOPUNOVIC: SIMBA SC NA COASTAL PATACHIMBIKA MKWAKWANI LEO

    Na Mahmoud Zubeiry, TANGA
    KOCHA wa Simba SC, Goran Kopunovic amesema mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania dhidi ya wenyeji wao, Coastal Union utakuwa mgumu.
    Coastal wanaikaribisha Simba SC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga jioni ya leo wakitoka kufungwa 1-0 na Yanga SC katikati ya wiki hapa hapa nyumbani.
    Na Mserbia anayefundisha Simba SC amesema kwamba hiyo pekee ni sababu tosha ya mchezo wa leo kuwa mgumu, kwa sababu Coastal hawatahitaji kufungwa mfululizo nyumbani.
    Lakini pia, Kopunovic amesema kwamba Uwanja mbaya wa Mkwakwani utawafanya washindwe kucheza mpira wao kiufundi, jambo ambalo litaongeza ugumu katika mchezo huo.
    Kocha wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic na Msaidizi wake, Suleiman Matola akijadiliana wakati wa mazoezi juzi Uwanja wa Mkwakwani

    Amesema alikuwepo uwanjani wakati Coastal inamenyana na Yanga SC na alishuhudia namna ambavyo mchezo ulivyokuwa mgumu wa kusukumana na kupamiana- anatarajia na leo itakuwa hivyo pia.
    “Hakutakuwa na ufundi, unaona hali ya huu uwanja, Coastal wana nguvu, tutapambana sana, itakuwa mechi ngumu. Lakini tutapigania ushindi,”amesema.     
    Kikosi cha Simba SC kiliwasili hapa Jumatano usiku na tangu Alhamisi kimekuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Mkwakwani.
    Katika mezoezi yake, Kopunovic amekuwa akiwapa mbinu za kutengeneza nafasi kwa mipira mirefu na kufunga.
    Na zaidi Mserbia huyo amekuwa akimuandaa mshambuliaji Mganda, Dan Sserunkuma kuwa mlaji wa mipira ya mwisho- maana yake ndiye aifungie mabao timu.
    Simba SC wamefanya mazoezi siku mbili mfululizo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
    Kocha Goran Kopunovic akimuelekeza Emmanuel Okwi namna ya kupiga mipira mirefu

    Tayari mshambuliaji huyo wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya ameonyesha anaweza baada ya kuifungia timu mabao matatu katika mechi nne za awali za Ligi Kuu alizocheza baada ya kusajiliwa Desemba. 
    Kiungo Said Ndemla anayesumbuliwa na maumivu ya nyama ataendelea kukosekana leo, wakati beki Nassor Masoud ‘Chollo’ tayari amejiunga na wenzake tangu mwanzoni mwa wiki. 
    Wachezaji wengine wote wa Simba SC, ukiondoa kipa Hussein Sharrif ‘Casillas’ majeruhi na kiungo Shaaban Kisiga ‘Malone’ aliyesusa wako fiti na wamefanya mazoezi vizuri wiki yote hii. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOPUNOVIC: SIMBA SC NA COASTAL PATACHIMBIKA MKWAKWANI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top