Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imetangaza viingilio vyao katika mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI ambapo kiingilio cha chini kabisa kikiwa ni shilingi 5000
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga Jerry Muro amesema wameamua kuweka kiwango hicho lengo likiwa ni kutaka kuwavuta mashabiki wengi.
Muro alisema mbali na 5000 viingilio vingine ni jukwaa la viti vya rangi ya chungwa ni shilingi 10000,VIP C 15000,VIP B 20000 huku VIP A shilingi 30000.
"Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wasitarajie mchezo huu kuuona katika luninga hatutaki kuruhusu hilo tunachiotaka tutatoa fursa kwa wale waliopo mikoani kuuona mchezo huu wakiwa huko lakini kwa wale wote waliopo katika mkoa huu hakutakuwa na matangazo ya mchezo huu,"alisema Muro.
"Tiketi hizi zitaanza kuuzwa mapema tutaanza kuuza siku moja kabla ya mchezo lakini pia tutoe taarifa fupi kuhusu hali ya kikosi chetu tulikuwa na wachezaji wawili ambao walikuwa majeruhi kipa wetu Deogratias Munishi 'Dida' na kiungo Haruna Niyonzima kwa sasa wapo safi tayari kwa mazoezi na wenzao."

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro akizungumza leo |
"Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wasitarajie mchezo huu kuuona katika luninga hatutaki kuruhusu hilo tunachiotaka tutatoa fursa kwa wale waliopo mikoani kuuona mchezo huu wakiwa huko lakini kwa wale wote waliopo katika mkoa huu hakutakuwa na matangazo ya mchezo huu,"alisema Muro.
"Tiketi hizi zitaanza kuuzwa mapema tutaanza kuuza siku moja kabla ya mchezo lakini pia tutoe taarifa fupi kuhusu hali ya kikosi chetu tulikuwa na wachezaji wawili ambao walikuwa majeruhi kipa wetu Deogratias Munishi 'Dida' na kiungo Haruna Niyonzima kwa sasa wapo safi tayari kwa mazoezi na wenzao."
0 comments:
Post a Comment