Na Mahmoud Zubeiry, TANGA
AFRICAN Sports ya Tanga imejihakikishia kurejea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya miaka 23, lakini imesema haitathamini tena udugu wao na Yanga SC.
Kisa? Sports wanadai Yanga SC haikuwa na msaada wowote kwao wakati wanasotea kurejea Ligi Kuu kwa miaka yote 23 na mbaya zaidi, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji aliwakana.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo mjini hapa, Meneja wa Sports, Abdul Ahmed Mohammed ‘Bosnia’ amesema kwamba Yanga SC wanatakiwa kufahamu kwamba udugu ni kufanana, bali ni kufaana.
“Katika kuhangaika kwetu turejee Ligi Kuu, sisi tulikwenda kuomba msaada Yanga SC, hawakutusaidia. Tena tuliandika barua hadi kwa Manji, jibu tulilopewa, eti Manji haitambui African Sports,”amesema Bosnia.
Meneja huyo amesema kwamba waliumia sana kukanwa na ndugu zao hao wa asili na damu, lakini wakaamua kupambana kwa namna nyingine hadi wamefanikiwa kurejea Ligi Kuu kwa msaada wa watu wengine.
“Coastal Union ni wapinzani wetu wa jadi hapa Tanga, lakini angalau wao walitusaidia katika vita yetu ya kupanda na tangu hapo tukaunda umoja wa “Tanga kwanza”. Kwa hiyo sasa hivi, timu za Tanga ni kitu kimoja kwa manufaa ya mkoa wa Tanga,”amesema.
Pamoja na hayo, Bosnia amesema udugu wa kihistoria baina yao na Yanga SC hauwezi kufa, isipokuwa hauna thamani tena baada ya kaka zao hao kuanza kutouthamini.
“Utabaki udugu wa kufanana kwa bendera na jezi, Wasitarajie msaada wowote kutoka kwetu, baada ya wao wenyewe kuanza kutukana. Hatumaanishi tumeua udugu, huo upo, lakini hauna thamani tena,”amesema.
Sports imejihakikishia kurejea Ligi Kuu baada ya kufikisha pointi 44 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine ya Kundi A, ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya JKT Mlale na Friends Rangers.

Meneja wa African Sports, Abdul Ahmed Mohammed 'Bosnia' akizungumza na BIN ZUBEIRY leo |
Wachezaji wa African Sports wakiwa mazoezini Uwanja wa sekondari ya Usagara mjini Tanga leo asubuhi |
“Katika kuhangaika kwetu turejee Ligi Kuu, sisi tulikwenda kuomba msaada Yanga SC, hawakutusaidia. Tena tuliandika barua hadi kwa Manji, jibu tulilopewa, eti Manji haitambui African Sports,”amesema Bosnia.
Meneja huyo amesema kwamba waliumia sana kukanwa na ndugu zao hao wa asili na damu, lakini wakaamua kupambana kwa namna nyingine hadi wamefanikiwa kurejea Ligi Kuu kwa msaada wa watu wengine.
“Coastal Union ni wapinzani wetu wa jadi hapa Tanga, lakini angalau wao walitusaidia katika vita yetu ya kupanda na tangu hapo tukaunda umoja wa “Tanga kwanza”. Kwa hiyo sasa hivi, timu za Tanga ni kitu kimoja kwa manufaa ya mkoa wa Tanga,”amesema.
Pamoja na hayo, Bosnia amesema udugu wa kihistoria baina yao na Yanga SC hauwezi kufa, isipokuwa hauna thamani tena baada ya kaka zao hao kuanza kutouthamini.
“Utabaki udugu wa kufanana kwa bendera na jezi, Wasitarajie msaada wowote kutoka kwetu, baada ya wao wenyewe kuanza kutukana. Hatumaanishi tumeua udugu, huo upo, lakini hauna thamani tena,”amesema.
Sports imejihakikishia kurejea Ligi Kuu baada ya kufikisha pointi 44 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine ya Kundi A, ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya JKT Mlale na Friends Rangers.
0 comments:
Post a Comment