• HABARI MPYA

    Thursday, February 06, 2014

    WAKOMORO WA YANGA WAANZA KUPASHA DAR

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam 
    KIKOSI cha timu ya Komorozine de Domoni kutoka Comoro leo jioni kinaanza rasmi mazoezi kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya wenyeji Yanga utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam keshokutwa.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY jijini Dar es Salaam mchana huu kuwa kikosi hicho ambacho kiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana jioni, kinafanya mazoezi yake ya kwanza nchini kwenye Uwanja wa Karume kuanzia saa 10:00 alasiri.

    "Leo jioni watakuwa kwenye Uwanja wa Karume, kesho jioni watakuwa Uwanja wa Taifa kama kanuni za mashindano zinavyoelekeza, timu kufanya mazoezi kwenye uwanja utakaochezewa mechi siku moja kabla ya mechi yenyewe," amaesema Wambura.
    Wakati Wacomoro hao wakijipanga kuanza kuandaa dozi leo jioni, wapinzani wao Yanga, wako mafichoni kambini mjini Bagamoyo, Pwani wakijifua kwa ajili ya mchezo huo wa hatua ya awali ya mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya klabu barabi Afrika.
    Timu itakayofuzu hatua hiyo baada ya kucheza mechi mbili nyumbani na ugenini, itachuana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly katika hatua ya pili.
    Yanga wanaonekana wazi kuibeza timu ya Komorozine inayotajwa kuwa kibonde kwani mpaka sasa wameshaingia ubia kwa kuuza matangazo ya moja kwa moja ya televisheni kwa dola za Marekani 55,000 (takriban Sh. milioni 90) na kampuni ya SGM kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya hatua ya pili dhidi ya Al Ahly itakayochezwa Uwanja wa Taifa.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAKOMORO WA YANGA WAANZA KUPASHA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top