• HABARI MPYA

    Saturday, February 08, 2014

    SIMBA SC KUWAFANYA KOMOROZINE WAJISIKIE WAPO NYUMBANI, YANGA WAKILALA NYUMBANI IMEKULA KWAO

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    IMEKUWA jambo la kawaida sasa, Simba SC inapocheza na timu yoyote hata ya nje ya nchi, mashabiki wa mahasimu wao, Yanga SC huingia uwanjani kwa wingi kuwashangilia wageni kuwapa nguvu wawafunge watani wao.
    Kadhalika na mashabiki wa Simba SC nao hujitokeza kwa wingi kwenye mechi za Yanga ili kushangilia wageni wawaadhiri watani wao.
    Burudani hiyo inatarajiwa Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Yanga itakapokuwa inamenyana na Komorozine ya Comoro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Ligi ya Mabingwa Afrika.

    Mashabiki wa Simba SC wanatarajiwa kumiminika kwa wingi na kujazana kwenye majukwaa yao kuwashangilia Wacomoro wawaadhiri mahasimu wao hao wa jadi.
    Kwa kawaida Simba SC na Yanga kama ilivyo kwa AC Milan na Inter Milan za Italia zinazotumia Uwanja mmoja San Siro kama wa nyumbani, nazo zinatumia Uwanja mmoja wa Taifa kama wa nyumbani kwa mechi zote.
    Timu hizo zimegawana majukwaa upande wa kulia wanakaa Yanga na kushoto wanakaa Simba SC.
    Hivyo Jumamosi hii, bila shaka mashabiki wa Simba SC watajazana kushoto mwa Uwanja wa Taifa kuwashangilia Komorozine dhidi ya Yanga watakaokuwa upande wa kulia.
    Hii inamaanisha kwamba Komorozine japokuwa itakuwa inacheza ugenini, lakini kwa hamasa na shangwe za wana Simba kwao, watajisikia kama wapo nyumbani.
    Inabidi mashabiki wa Yanga nao waende kwa wingi Uwanja wa Taifa ili kuzifunika shangwe za wana Simba SC, vinginevyo wachezaji wao watakuwa wanyonge.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC KUWAFANYA KOMOROZINE WAJISIKIE WAPO NYUMBANI, YANGA WAKILALA NYUMBANI IMEKULA KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top