• HABARI MPYA

    Sunday, February 09, 2014

    MBEYA CITY YAISHUSHA SIMBA SC ‘ILIYOPAKATWA’ MKWAKWANI

    Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam na mikoani
    MBEYA City imezinduka jioni ya leo baada ya kuilaza mabao 2-1 Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Peter Michael dakika ya pili na Hamad Kibopile dakika ya 67, wakati la Mtibwa limefungwa na Jamal Mnyate dakika ya 53.
    Mbeya City sasa wanatimiza pointi 34 na kurejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Yanga SC pointi 35 na Azam FC 36.
    Kikosi cha Mbeya City

    Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora bao pekee la Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ dakika ya nane limeipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Rhino Rangers.
    Kagera Sugar wamelazimisha sare ya 1-1 ugenini Uwanja wa Sheikh Amri Abeid dhidi ya wenyeji JKT Oljoro. Bao la Kagera limefungwa na Themi Felix dakika ya saba na Oljoro wakasawazisha kupitia kwa Jacob Masawe dakika ya 82.
    Tanga bao pekee la Fully Maganga dakika ya 29 limeipa Mgambo JKT ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba SC.
    Mapema jana Tanzania Prisons iliifunga mabao 3-1 Ruvu Shooting, mabao yake yakitiwa kimiani na Michael Peter dakika ya 56, Jeremiah Juma dakika ya 85 na Laurian Mpalile dakika ya 89 ambaye alijifunga pia dakika ya 85 kuwapatia wapinzani wao bao la kufutia machozi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAISHUSHA SIMBA SC ‘ILIYOPAKATWA’ MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top