• HABARI MPYA

    Friday, June 04, 2021

    UONGOZI WA AZAM FC WAZURU UBALOZI WA ZIMBABWE NCHINI KWA MWALIKO WA BALOZI ALIYEFURAHISHWA NA USAJILI WA WACHEZAJI KUTOKA KWAO

     UONGOZI wa Azam FC leo umetembelea Ubalozi wa Zimbabwe hapa nchini kwa mwaliko maalumu kutoka kwa Balozi wa nchi hiyo, Luteni Generali Mstaafu, Anslom Sanyatwe.
    Viongozi wa Azam FC, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Omary Kuwe na Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', waliongoza msafara mzima ulioambatana wachezaji wa timu hii kutoka nchini Zimbabwe.
    Wachezaji hao ni mshambuliaji kinara, Prince Dube, beki kisiki wa kushoto, Bruce Kangwa, kiungo machahari, Never Tigere, sambamba na Mtaalamu wa sayansi ya michezo, Nyasha Charandura.


    Balozi huyo aliipongeza Azam FC kwa kutoa nafasi kwa wachezaji kutoka Zimbabwe, huku akiwataka wachezaji hao kutumia vema nafasi hiyo kwa kupeperusha vyema bendera ya nchi hiyo na kuisaidia timu hiyo ya Tanzania.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UONGOZI WA AZAM FC WAZURU UBALOZI WA ZIMBABWE NCHINI KWA MWALIKO WA BALOZI ALIYEFURAHISHWA NA USAJILI WA WACHEZAJI KUTOKA KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top