UGANDA wamefanikiwa kwenda fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Tunisia jana Uwanja wa Olimpiki wa Nouakchott.
Nyota wa mchezo wa jana alikuwa Derrick Kakooza aliyepiga hat trick kwa mabao yake ya dalkika za 36, 50 na 73 huku lingine likifungwa na Richard Basangwa dakika ya nne na la Tunisia lilifungwa na Adam Ben Lamin dakika ya 39.
Sasa The Hippos 'Kiboko' wanaingia fainali itakayochezwa Jumamosi na watamenyana na Ghana 'Black Satellites' iliyoichapa Gambia 1-0 jana, bao pekee la Percious Boah dakika ya 34.
0 comments:
Post a Comment