KIPA Mohamed El Shenaway jana aliokoa penalti mbili kuiwezesha Al Ahly kumaliza nafasi ya tatu Klabu Bingwa wa Dunia baada ya ushindi wa penalti 3-2 kufuatia sare ya 0-0 na Palmeiras ya Brazil Uwanja wa Education City mjini Al Rayyan, Qatar.
El Shenaway aliokoa penalti za Rony na Felipe Melo, huku Luiz Adriano naye kukosa, wakati Gustavo Scarpa na Gustavo Raúl Gomez pekee waliifungia Palmeiras, Al Ahly wakibeba Medaliza Shaba.
Waliofunga penalti za Al Ahly ni Badr Banoun, Mohamed Hany na Oluwafemi Junior Ajayi huku Amr Al Sulaya na Marwan Mohsen wakikosa.
0 comments:
Post a Comment