• HABARI MPYA

    Friday, October 23, 2020

    MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI LIGI KUU TANZANIA BARA KUJIUNGA NA MACCABI TEL-AVIV YA ISRAEL

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MCHEZAJI Bora Chipukizi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Novatus Dismas atajiunga na klabu ya Maccabi Tel-Aviv ya Israel baada ya kufuzu majaribio.
    Taarifa ya klabu yake, Azam FC leo imesema kwamba wamefikia makubaliano ya kumuuza kiungo wao huyo chipukizi Maccabi Tel-Aviv.
    "Dismas anajiunga na timu hiyo baada ya Maccabi kuvutiwa na uwezo wake kwa kipindi cha takribani cha mwezi mmoja alichofanya majaribio ndani ya timu hiyo ambayo imekuwa ikishiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA)," imesema taarifa ya Azam FC.


    Novatus anakuwa mchezaji wa pili kuuzwa na Azam FC msimu hu, baada ya wiki chache zilizopita kumpiga bei mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda, aliyejiunga na Mouloudia d'Oujda ya Morocco.
    Dismass amekuzwa kwenye kituo cha kukuza vipaji cha Azam FC sambamba na Chilunda kabla ya wote kupandishwa timu kubwa kwa wakati tofauti.
    Azam FC imesema itaendelea kuthamini na kuendeleza vipaji vya wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cheke na haitasita kufanikisha ndoto zao za kwenda kucheza nje ya nchi pale mchezaji anapopata timu na taratibu zote zinapofuatwa na timu husika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI LIGI KUU TANZANIA BARA KUJIUNGA NA MACCABI TEL-AVIV YA ISRAEL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top