• HABARI MPYA

    Sunday, August 16, 2020

    UTAMBULISHO WA JEZI ZA MSIMU MPYA AZAM FC ULIVYOFANA LEO KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA CHAMAZI

    Wachezaji wa Azam FC kutoka kulia, beki Aggrey Morris, kiungo Iddi Suleiman 'Nado', mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa na kiungo Mzimbabwe, Never Tegere wakiwa wamevaa jezi mpya za klabu hiyo za msmu mpya ambazo tayari zinapatikana sokoni kwa kwa bei poa kabisa ya Sh. 20,000 kwenye duka la klabu la Kariakoo 'Azam FC Sports Shop' na uwanjani Azam Complex. Jezi nyeupe itakuwa ya nyumbani, bluu itakuwa ya ugenini huku ya orange ikiwa ya ziada (neutral). 
    Mara baada ya uzinduzi, jezi zimeanza kuuzwa leo Uwanja wa Azam Complex na pia zitapatikana dukani la klabu, Kariakoo, Dar es Salaam
    Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau, akitambulisha jezi rasmi za Azam FC za msimu ujao. Kidau mbali na kutambulisha jezi pia ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa wiki ya Chamazi iliyoanza rasmi leo, ambayo itaitimika Jumapili ijayo kwa Tamasha la Azam Festival.
     Wiki ya Chamazi ndani ya Azam Complex.
     Wiki ya Chamazi ndani ya Azam Complex.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UTAMBULISHO WA JEZI ZA MSIMU MPYA AZAM FC ULIVYOFANA LEO KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top