• HABARI MPYA

  Friday, August 14, 2020

  POULSEN AISAIDIA LEIPZIG KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

  MSHAMBULIAJI Mdenmark mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Yurary Poulsen (kushoto) jana ameisaidia RB Leipzig kutinga Nusu Fainali ya UEFA Champions League baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Atletico Madrid ya Hispania usiku wa jana Uwanja wa Jose Alvalade Jijini Lisbon, Ureno.
  Daniel Olmo alianza kuifungia RB Leipzig dakika ya 50 kabla ya Joao Felix kusawazisha kwa penalty dakika ya 71 na Tyler Adams kufunga la ushindi dakika ya 88.
  RB Leipzig sasa itamenyana na wababe wa Atalanta ya Italia, PSG katika Nusu Fainali Agosti 18 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POULSEN AISAIDIA LEIPZIG KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top