• HABARI MPYA

    Monday, August 17, 2020

    AZAM FC YAMSAJILI MSHAMBULIAJI MZIMBABWE, PRINCE DUBE KUTOKA HIGHLANDERS YA BULAWAYO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Azam FC imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube kutoka Highlanders  FC ya Bulawayo, nchini kwao.
    Dube ambaye ni mmoja ya washambuliaji hatari Zimbabwe, akiwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo cha wachezaji wa ndani, ambaye anakuja Azam FC kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.
    Benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, limeridhishwa kwa kiasi kikubwa na uwezo wake kwa muda wote waliomfuatilia hadi kuamua kumsajili.
    Huo unakuwa usajili wa saba kwenye kikosi cha Azam FC, katika dirisha hili la usajili kwa ajili ya msimu ujao, wengine wakiwa ni kipa David Kissu, beki wa kushoto Emmanuel Charles.
    Wachezaji wengine walioongezwa ni kiungo mkabaji, Ally Niyonzima, viungo washambuliaji, Awesu Awesu, Ismail Aziz na Ayoub Lyanga.
    Zoezi letu la usajili tutalifunga hivi karibuni kwa kumsajili mshambuliaji mwingine wa kimataifa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAMSAJILI MSHAMBULIAJI MZIMBABWE, PRINCE DUBE KUTOKA HIGHLANDERS YA BULAWAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top