• HABARI MPYA

    Tuesday, February 11, 2020

    MUDATHIR AREJEA KUTOKA ULAYA NA KUIFUNGIA BAO PEKEE AZAM FC IKIICHAPA 1-0 POLISI TZ

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BAO la dakika ya 48 la kiungo Mudathir Yahya Abbas limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania jioni ya Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
    Mudathir alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza Azam FC baada ya kurejea kutoka Latvia alipokwenda kufanya majaribio katika klabu ya Riga FC.
    Kwa ushindi huo, Azam FC imefikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 21, ikiendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 53 sasa za mechi 21 pia. 
    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, mabao ya John Bocco, Mohammed Hussein na Hassan Dilunga yaliipa Simba SC ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

    Bao pekee la Atupele Green dakika ya 63 lilitosha kuwapa Biashara United ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
    Uwanja wa Liti mkoani Singida, bao pekee la Zingamasebo Steven dakika ya 68 likaipa Namungo FC ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Singida United.
    Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, mabao ya Samuel John dakika ya 69 na Omary Khamis dakika ya 89 yakaipa ushindi wa 2-0 Ndanda FC dhidi ya wenyeji, Mwadui FC.
    Kagera Sugar wakakubali kichapo 2-1 nyumbani mbele ya Alliance FC ya Mwanza Uwanja wa Kaitaba mkoani Bukoba mabao ya wageni yakifungwa na Martin Kigi dakika ya 64 na David Richard dakika ya 90 na ushei huku bao pekee la wenyeji likifungwa Nassor Kapama dakika ya 90. 
    Lipuli FC ikalazimishwa sare ya 1-1 na JKT Tanzania Uwanja wa Samora mkoani Iringa tena yenyewe ikisawazisha kupitia kwa Issah Ngoah dakika ya 17 baada ya Edson Katanga kuanza kuwafungia wageni dakika ya tano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUDATHIR AREJEA KUTOKA ULAYA NA KUIFUNGIA BAO PEKEE AZAM FC IKIICHAPA 1-0 POLISI TZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top