• HABARI MPYA

    Friday, January 10, 2020

    AZAM FC NA FRIENDS RANGERS, SIMBA NA MWADUI FC NA YANGA DHIDI YA PRISONS RAUNDI YA NNE ASFC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MABINGWA watetezi, Azam FC watamenyana na timu ya Daraja la Kwanza, Friends Rangers katika Raundi ya Nne ya Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
    Katika droo ya hatua hiyo iliyopangwa leo ofisi za Azam TV, Tabata Jijini Dar es Salaam, vigogo Simba na Yanga wameangukiwa kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ingawa wote watacheza nyumbani kama Azam FC.
    Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba SC watamenyana na Mwadui FC ya Shinyanga na washindi mara nyingi zaidi wa taji la Ligi Kuu, Yanga SC Africans watamenyana na Tanzania Prisons.

    Upangaji wa ratiba ya Raundi ya Nne ambayo mechi zake zitachezwa kuanzia Januari 24 hadi 26 mwaka, kwa ujumla umehusisha timu 64 za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza, Daraja la Pili na zinazoshiriki Ligi za Mikoa.
    Ikivuka hatua hiyo, Raundi ya Tano Azam FC itasafiri kumfuata mshindi kati ya Ihefu na Gipco, sawa na Simba ambayo itamfuata mshindi kati ya Maji Maji na Stand United, wakati Yanga itabaki nyumbani kwa ajili ya kumenyana na mshindi kati ya Gwambina na Ruvu Shooting.
    Mechi nyingine za Raundi ya Nne ni Gwambina dhidi ya Ruvu Shooting, African Sports dhidi ya Alliance, Polisi Tanzania dhidi ya Mbeya City, Ndanda FC dhidi ya Dodoma FC, Majimaji FC dhidi ya Stand United, Ihefu FC dhidi ya Gipco FC na KMC dhidi ya Pan Africans.
    Nyingine ni Panama FC na Mtwivila FC, Namungo FC na Biashara United, Mtibwa Sugar na Sahare All Stars, JKT Tanzania na Tukuyu Stars, Kagera Sugar na Might Elephant, Lipuli FC na Kitayosa.
    Awali droo hiyo iliyoongozwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi iliuteua Uwanja wa kumbukumbu ya Nelson Mandela mkoani Rukwa kuwa wenyeji wa Fainali ya michuano hiyo Mei 30, mwaka huu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC NA FRIENDS RANGERS, SIMBA NA MWADUI FC NA YANGA DHIDI YA PRISONS RAUNDI YA NNE ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top