• HABARI MPYA

    Wednesday, November 06, 2019

    SAMATTA AINYAMAZISHA ANFIELD KWA MUDA BAADA YA KUIPIGA LIVERPOOL BAO LA KICHWA

    Na Mwandishi Wetu, LIVERPOOL
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samata jana ameifungia bao timu yake, KRC Genk ikichapwa 2-1 na wenyeji, Liverpool katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Anfield.
    Samatta aliyekuwa anacheza Anfield kwa mara ya kwanza, aliifungia KRC Genk bao hilo dakika ya 40 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo Mbelgiji, Bryan Heynen.
    Na hiyo ilifuatia mabingwa wa Ulaya, Liverpool kutangulia kwa bao la Georginio Wijnaldum dakika ya 14 akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya KRC Genk.
    Mbwana Samata akikimbia kushangilia baada ya kuifungia KRC Genk jana Uwanja wa Anfield

    Mbwana Samata aliruka kwenye msitu wa mabeki wa Liverpool kufunga bao hilo

    Alex Oxlade-Chamberlain akaifungia Liverpool bao la ushindi dakika ya 53 akimalizia pasi ya Mohamed Salah na kwa ushindi huo timu y Jurgen Klopp inaongoza Kundi E kufuatia Napoli kutoa sare na Salzburg jana.
    Samatta jana amecheza mechi ya ya 173 jumla kwenye mashindano yote tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amefunga mabao 69.
    Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya hiyo inakuwa mechi ya nne akiwa amefunga mabao mawili sasa, ligi ya Ubelgiji mechi 135 na mabao 53, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja na Europa League mechi 24 na mabao 14.
    Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Alisson, Alexander-Arnold, Gomez, van Dijk, Milner, Wijnaldum, Fabinho, Keita/Robertson dk73, Oxlade-Chamberlain/Mane dk74, Salah, Origi/Firmino dk88.
    KRC Genk; Coucke, Cuesta, Dewaest, Lucumi, Maehle, Heynen, Berge, Hrosovsky/Bongonda dk84, De Norre/Onuachu dk84, Ito/Ndongala dk68 na Samatta.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AINYAMAZISHA ANFIELD KWA MUDA BAADA YA KUIPIGA LIVERPOOL BAO LA KICHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top