• HABARI MPYA

  Saturday, October 05, 2019

  AZAM FC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA NAMUNGO FC 2-1 CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Namungo FC 2-1 usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa kiungo mkongwe wa timu hiyo, Frank Raymond Domayo aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90 kwa shuti la kipimo kufuatia krosi ya beki Mganda, Nicolas Wadada.
  Lakini haukuwa ushindi mwepesi, kwani Azam FC ililazimika kutoka nyuma baada ya kutanguliwa na Namungo FC ambao bao lao lilifunga na mchezaji wao machachari, Lucas Kikoti dakika ya 48.
  Mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Dondo Ngoma akaisawazishia Azam FC dakika ya 61 akimalizia kazi nzuri ya Wadada pia.
  Baada ya mchezo wachezaji wa Namungo FC walimvamia refa Omar Mdoe kutoka Tanga na wasaidizi wake, Kassim Safisha wa Pwani na Abdulaziz Ally wa Arusha kuwalalamikia kabla ya kudhibitiwa na walinzi.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja tu, Yanga SC wakiwakaribisha Coastal Union Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, wakitoka kucheza mechi nne mfululizo bila ushindi, ikitoa sare mbili na kufungwa mbili.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammd, Daniel Amoah, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Donald Ngoma/Obrey Chirwa dk62, Daly Ella Richard Djodi na Iddi/Emmanuel Mvuyekure dk71 Suleiman ‘Nado’/Shaaban Idd Chilunda dk59.  
  Namungo FC; Nurdine Balora, Miza Cristom, Ally Suleiman, Stephen Duah, Hamisi Fakhi, Carlos Protas/John Mbise dk84, Hashimu Manyanya, Nzigamasaba Steve, Omar Mponda/Jerome Sina dk56, Lucas Kikoti na George Makang’a.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA NAMUNGO FC 2-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top