• HABARI MPYA

    Sunday, September 01, 2019

    AMBAYE HAJACHEZA SOKA WALA KUFUNDISHA KLABU KUBWA AWA KOCHA MKUU BAFANA

    AFRIKA Kusini imeteua Molefi Ntseki, ambaye hajawahi kucheza soka ya kulipwa au kufundisha klabu kubwa kuwa Kocha Mkuu wake mkuu baada ya kujiuzulu kwa Muingereza, Stuart Baxter mwezi uliopita.
    Uteuzi huo wa kushangaza umetangazwa leo kwenye Twitter na Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji mjini Johannesburg.
    Ntseki, aliyekuwa Msaidizi wa Baxter kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri ambako Afrika Kusini ilifika Robo Fainali, ameteuliwa kuwa kocha wa muda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zambia mwishoni mwa wiki ijayo.
    Lakini makocha wa klabu kubwa walitarajiwa kupewa kazi hiyo kwa mikataba rasmi wakiwemo Benni McCarthy wa Cape Town City, Gavin Hunt wa Bidvest Wits na Steve Komphela wa Golden Arrows.  
    McCarthy na Komphela ni nyota wa zamani wa timu ya taifa na Hunt ameshinda mataji ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa rekodi,mara nne kama kocha.
    Zaidi ya kumsaidia Baxter na makocha wengine wawili wa zamani wa timu ya taifa, Mwalimu huyo wa zamani wa shule alikuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17.
    Mtihani wake wa kwanza mkubwa utakuwa mwezi Novemba Afrika Kusini itakapowafuata wenyeji, Ghana na wenyeji, Sudan kwenye mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2021.
    Baxter alijiuzulu miaka mitatu kabla ya kumaliza mkataba wake, akisema anaamini anachokifanya hakina thamani ya mbele ya viongozi wa soka, jamii na vyombo vya Habari Afrika Kusini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMBAYE HAJACHEZA SOKA WALA KUFUNDISHA KLABU KUBWA AWA KOCHA MKUU BAFANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top