• HABARI MPYA

  Saturday, July 06, 2019

  AMBOKILE ATUA NA KIKOSI CHA TP MAZEMBE KIGALI TAYARI KUSHIRIKI KOMBE LA KAGAME

  Na Mwandishi Wetu, LUBUMBASHI
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Eliud David Ambokile ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na TP Mazembe kwenda Rwanda kwenye michuano ya Kombe la Kagame.
  Taarifa ya Mazembe imesema kwamba, kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na timu hiyo kutoka Mbeya City ya nyumbani, Tanzania ataanza kazi mara moja.
  “Katika safari ya Kigali ambako The Ravens wanatarajiwa kucheza michuano ya Cecafa Kagame, mchezaji huyo atakuwepo kwenye msafara baada ya kujiunga na timu Lubumbashi,.”imesema taarifa ya TP Mazembe.

  Mazembe inataka kujaribu tena kuwekeza kwa chipukizi huyo wa Tanzania baada ya kuvuna matunda kwa Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu.
  Wawili hao waliitumikia Mazembe kwa mafanikio kuanzia mwaka 2011 kabla ya wote kuondoka wakifuatana, Samatta akianza 2016 kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji na Ulimwengu akifuatia 2017 kujiunga na AFC Eskilstuna ya Sweden kabla ya kuhamia, FK Sloboda Tuzla ya Bosnia, Al-Hilal ya Sudan mwaka 2018 na sasa JS Saoura ya Algeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMBOKILE ATUA NA KIKOSI CHA TP MAZEMBE KIGALI TAYARI KUSHIRIKI KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top