• HABARI MPYA

  Friday, June 21, 2019

  TORRES ASTAAFU RASMI SOKA BAADA YA MIAKA 18 YA MAFANIKIO

  Fernando Torres ametangaza kustaa soka baada ya miaka 18 ya mafanikio 


  KABATI LA MATAJI LA FERNANDO TORRES: 

  Kombe la Dunia - 2010
  Euro - 2008, 2012
  Ligi ya Mabingwa Ulaya - 2011-12
  Europa League - 2012-13, 2017-18
  Kombe la FA - 2011-12
  GWIJI wa Hispania, mshambuliaji Fernando Torres ametangaza kustaa soka baada ya miaka 18 ya mafanikio.
  "Nina kitu fulani muhimu sana cha kutangaza, baada ya miaka 18 ya kuvutia, wakati wa kumaliza kucheza soka umefika," amesema Torren.
  Torres anaacha soka akiwa ana umri wa miaka 35,  kwenye klabu ya Sagan Tosu ya Japan aliyojiunga nayo akitokea Atletico Madrid mwaka jana.
  Enzi zake alifunga mabao 81katika misimu minne ya kucheza England, akiiwezesha Liverpool kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kuipa Chelsea mataji ya Europa League na Kombe la FA. 
  Katika soka ya kimataifa aliipa Hispania mataji mawili ya Euro mwaka 2008 na 2010 na Kombe la Dunia 2010.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TORRES ASTAAFU RASMI SOKA BAADA YA MIAKA 18 YA MAFANIKIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top