• HABARI MPYA

  Friday, June 07, 2019

  AHMAD ATIWA MBARONI UFARANSA KWA TUHUMA ZA UFISADI

  RAIS wa Shirikisho la SokaAfrika (CAF), Ahmad ametiwa mbaroni na mamlaka nchini Ufaransa ambako alikuwa akihudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
  Taarifa ya kukamatwa kwake imethibitishwa na FIFA lakini haijaweka wazi sababu zaidi ya kusema “Tuhuma zake zinahusiana na mamlaka yake akiwa Rais wa CAF”.
  Taarifa hiyo imeongeza kuwa “FIFA haijui kwa undani uchunguzi unaofanywa dhidi yake kwahiyo haiwezi kusema chochote”.

  Rais wa CAF, Ahmad (kulia) ametiwa mbaroni na mamlaka nchini Ufaransa alipokuwa akihudhuria Mkutano Mkuu wa FIFA

  FIFA imeziomba mamlaka zinazohusika na sakata hilo nchini Ufaransa kutoa taarifa kwenye kamati yake ya maadili.
  Ahmad Ahmad raia wa Madagascar amekamatwa ikiwa siku moja baada ya kuongoza kikao cha kamati ya utendaji ya CAF iliyoamuru kurudiwa kwa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Esperance na Wydad Casablanca baada ya kubainika kuwa ilikuwa na ukiukwaji wa taratibu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AHMAD ATIWA MBARONI UFARANSA KWA TUHUMA ZA UFISADI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top