• HABARI MPYA

  Tuesday, June 04, 2019

  LEWIS AMSHAURI JOSHUA KUFUKUZA KOCHA BAADA YA KIPIGO RUIZ

  BINGWA wa zamani wa dunia wa ngumi za kulipwa uzito wa juu, Lennox Lewis amemshauri Anthony Joshua kumfukuza kocha wake Rob McCracken baada ya kipigo kikali kutoka kwa Andy Ruiz.
  McCracken alimuwezesha Joshua kutwaa Medali ya Dhahabu ya Olimpiki kabla ya kumpa mataji ya dunia ya ngumi za kulipwa ya IBF, WBA and WBO, lakini Lewis anaamini mabadiliko makubwa yanahitajika baada ya matokeo mabaya ya Jumamosi ukumbi wa Madison Square Garden.
  Lewis, ambaye alibadili kocha na kumchukua Manny Steward baada ya kupigwa na Oliver McCall mwaka 1994, amesema: "Nasema huwezi kwenda Chuo Kikuu na Mwalimu wako wa Daraja la Tatu. Hawawezi kuwa na majibu unayoyahitaji katika kiwango hicho. Utahitaji profesa wakati huo.

  Lennox Lewis amemshauri Anthony Joshua kubadili kocha  baada ya kipigo cha Andy Ruiz 

  "McCracken ni daraja la kwanza A bila swali, lakini labda hatoshelezi kwa staili anayohitaji AJ kupigana. Nilihamia kwa Manny Steward ambaye alikuwa anaelewa zaidi nguvu na kipaji changu na akanionyesha kila nilichohitaji kujua ili kufanikiwa,".
  Lewis amesema: "Yeye (McCracken) anaweza kuwa si sahihi kwa aina ya staili ambayo AJ anahitaji kuielewa. Mbali na hiyo, AJ hakujiandaa kwa chochote alichokuja nacho mezani Ruiz,".
  Hii si tathmini nzuri kwa McCracken ambaye amemuinua Joshua kwenye mchezo huo kuanzia ngumi za Ridhaa hadi za kulipwa na ambaye pia alimfundisha kwa mafanikio makubwa Carl Froch. 
  Hata hivyo, kuna dalili zozote za kubadili kocha hadi sasa katika kambi ya Joshua.
  Ushauri wa Lewis unakuja wakati Eddie Hearn amekanusha taarifa kwamba Joshua aliangushwa katika pambano la mazoezi wiki chache kabla ya pambano la Jumamosi. 
  Ilielezwa kwamba alidondoshwa na Agit Kabayel, bingwa wa Ulaya, ambaye pia ilidaiwa alimuachia alama Joshua usoni iliyoonekana hata kabla ya kupigwa na Ruiz.
  Lakini Hearn amesema kwamba Joshua hakuangushwa na hata mmoja kati ya mabondia aliopigana nao mapambano ya mazoezi na kwamba wala Kabayel hakuwa miongoni mwao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LEWIS AMSHAURI JOSHUA KUFUKUZA KOCHA BAADA YA KIPIGO RUIZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top