• HABARI MPYA

  Monday, June 03, 2019

  KAGERA SUGAR YALAZIMISHA SARE 0-0 NA PAMBA NYAMAGANA, MWADUI NAYO YAIBANA GEITA

  Na Asha Said, MWANZA
  TIMU ya Kagera Sugar imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kulazimisha sare ya 0-0 na wenyeji Pamba SC jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Mchezo huo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kubaki na kupanda Ligi Kuu, ulikuwa mkali na wa kusisimua na Pamba SC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi walizotengeza.
  Sasa Kagera Sugar wanarejea nyumbani Bukoba kujipanga kwa mchezo wa marudiano Jumamosi Uwanja wa Kaitaba, wakihitaji ushindi ili kusalia Ligi Kuu.
  Kagera Sugar wameangukia katika Play-Off baada ya kumaliza nafasi ya 18 kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wakati Pamba SC ilimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi B.
  Mchezo mwingine wa kwanza wa mchujo wa kuwania kubaki na kupanda Ligi Kuu, wenyeji Geita Gold Mine wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mwadui FC Uwanja wa Nyankungu, Geita.
  Mwadui FC ilimaliza nafasi ya 17 katika Ligi Kuu ya Tanzania iliyomalizika wiki iliyopita, wakati Geita ilishika nafasi ya pili Kundi A Daraja la Kwanza.
  Ikumbukwe Polisi Tanzania ya Kilimanjaro iliyoongoza Kundi B na Namungo FC ya Lindi iliyoongoza Kundi A zimepanda moja kwa moja Ligi Kuu, wakati African Lyon iliyoshika mkia Ligi Kuu na Stand United iliyomaliza nyuma yao, nafasi ya 19 zimeshuka moja kwa moja.  
  Kikosi cha Pamba SC kilikuwa; Deus Tilusubya, Hassan Kabailo, Amos Ikuzungura, Alex Joseph, John Mtobesya, Salum Ally, Yussuf Dunia, Salum Juma, Shija Mkina, Elias Seth/Kelvin John dk69 na Ally Rajab/David Richard dk84. 
  Kagera Sugar; Ramadhani Chalamanda, Mwaita Gereza, David Luhende, Juma Nyosso, JUma Shemvuni, Peter Mwalyanzi, Suleiman Mangoma, Ally Ramadhani, Ramadhani Kapera, Paul Ngalyoma/Jerson Tegete dk68 na Venende Ludovic/Japhet Makalai dk53.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YALAZIMISHA SARE 0-0 NA PAMBA NYAMAGANA, MWADUI NAYO YAIBANA GEITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top