• HABARI MPYA

  Wednesday, June 05, 2019

  AZAM FC YAMTHIBITISHA NDAYIRAGIJJE KUWA KOCHA WAKE MPYA, MATOLA ANAKWENDA KMC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Azam FC upo mbioni kumalizana na Kocha Mkuu wa KMC ya Kinondoni,Etienne Ndayiragije kurithi nafasi ya Hans van set Pluijm aliyondolewa kukinoa kikosi cha timu hiyo.
  Azam walimuondoa Pluijm na msaidizi wake baada ya timu hiyo kutofanya vizuri na badala yake timu hiyo ilikuwa chini ya makocha wazawa Abdul Mingange na Iddi Cheche.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana mjini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin 'Popat' alisema wapo katika mazungumzo ya mwisho Na muda wowote atasaini mkataba kukinoa kikosi chai.

  Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin 'Popat'(kulia) amesema wanamleta Ndayiragijje

  "Ni kweli tuko katika mazungumzo ya mwisho na kocha wa KMC hivyo baada ya kukamilika kila kitu kutakuwa wazi, suala la usajili pia tunasubiri baada ya kusaini mkataba ndio aendelee na mchakato huo," alisema Popat.
  Wakati huo huo: Kocha wa Lipuli FC ya Iringa, Suleiman Matola anatajwa kwenda kuchukua nafasi ya Ndayiragijje KMC.
  Baada ya kuifikisha Lipuli FC fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Matola ambaye Nahodha wa zamani wa klabu ya Simba ameitwa na na Halmashauri ya Manipsaa ya Kinondoni mjini Dar es Salaam kuhamishia ujuzi wake KMC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMTHIBITISHA NDAYIRAGIJJE KUWA KOCHA WAKE MPYA, MATOLA ANAKWENDA KMC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top