• HABARI MPYA

  Tuesday, June 04, 2019

  ALLY NG’ANZI ATOLEWA KWA MKOPO NA MAREKANI, APELEKWA TIMU YA DARAJA LA TATU

  Na Mwandishi Wetu, WISCONSIN 
  KIUNGO chipukizi Mtanzania, Ally Hamisi Ng'anzi ametolewa tena kwa mkopo kutoka klabu ya Minnesota United FC ya Ligi Kuu ya Marekani ijulikanayo kama MLS kwenda Forward Madison FC ya Daraja la Tatu, ijulikanayo kama USL League One.
  Ikumbukwe Ng'anzi mwenye umri wa miaka 18 alijiunga na Minnesota United FC kwa mkopo pia Machi mwaka huu kutoka Vyskov ya Daraja la Tatu Jamhuri ya Czech iliyomsajili kutoka SIngida United ya nyumbani kwao mwaka jana mwishoni.
  Kisoka Ng'anzi maarufu kwa jina la utani Ally Pasi kutoka na utoaji wake pasi nzuri na za uhakika aliibukia akademi ya Shule ya Alliance mjini Mwanza ambayo ilimfanya aonekane timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2016.
  Ally Ng'anzi ametolewa tena kwa mkopo kutoka Minnesota United FC kwenda Forward Madison FC

  Ally Ng'anzi (chini) katika moja ya mechi alizocheza nchini Marekani 

  Alikuwemo kwenye kikosi cha Serengeti Boys kilichofuzu na kushiriki fainali za U17 nchini Gabon mwaka 2017 na baada ya michuano hiyo akasajiliwa na Singida United ikiwa chini ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kabla ya mwishoni mwa mwaka jana kuuzwa Vyskov.
  Katika timu ya Forward Madison FC yupo na mchezaji mwingine Mtanzania, Vital Nizigiyimana kiungo pia kama Waafrika pekee kwenye kikosi hicho cha kocha Mmarekani, United States Daryl Shore.
  Forward Madison FC ni timu mpya yenye maskani yake Madison, Wisconsin ambayo imeanzishwa mwaka jana tu ikitumia Uwanja wa Breese Stevens Field kwa mechi zao za nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALLY NG’ANZI ATOLEWA KWA MKOPO NA MAREKANI, APELEKWA TIMU YA DARAJA LA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top