• HABARI MPYA

    Saturday, May 04, 2019

    MBARAKA IGANGULA AJIONDOA KUGOMBEA NAFASI YA UENYEKITI WA KLABU YA YANGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MGOMBEA Uenyekiti katika uchaguzi wa klabu ya Yanga unaofanyika kesho, Mbaraka Igangula amejitoa na kumuacha Dk. Mshindo Msolla anayepewa nafasi kubwa ya kushinda kwenye mazingira makubwa ya kuwa kiongozi mpya mkuu wa klabu hiyo.
    Igangula ametoa waraka wa kujitoa leo na kumuacha sasa Msolla abaki anapambana na Elias Mwanjala, Dk. Jonas Benedict Tiboroha, na Erick Ninga kuwania Uenyekiti wa klabu ya Yanga katika uchaguzi uliopangwa kufanyika kesho mjini Dar es Salaam.
    Nafasi ya Makamu Mwenyekiti inawaniwa na Katibu wa zamani wa TFF, Frederick Wilfred Mwakalebela na Mbunge wa jimbo Ileje (CCM) Mheshimiwa, Janet Zebedayo Mbena, Yono Kevela, Titus Eliakim Osoro na Salum Magege Chota.
    Dk. Mshindo Msolla anapewa nafasi kubwa ya kushinda Uenyekiti wa klabu ya Yanga

    Nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji zinawaniwa na Dominick Albinus, Saad Mohamed Khimji, Hassan Yahya Hussein, Shafiru Amour Makosa, Mhandsi Bahati Faison Mwaseba, Hamad Ali Islam, Mhandisi Leonard Marangu, Suma Mwaitenda na Haruna Hussein Batenga. 
    Wengine 16 ni Hamad Ally Islam, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Shafil Amri, Said Kambi, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka na Athanas Peter Kazige.  
    Uchaguzi huu unafuatia kujiuzulu kwa viongozi wote waliongia madarakani Juni 11 mwaka 2016, Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wao, Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay, Hussein Nyika, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Inspekta Hashim Abdallah.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBARAKA IGANGULA AJIONDOA KUGOMBEA NAFASI YA UENYEKITI WA KLABU YA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top