• HABARI MPYA

  Monday, April 08, 2019

  TWIGA STARS WAJINOA MARA YA MWISHO LEO KABLA YA KURUDIANA NA DRC KESHO KINSHASA

  Na Mwandishi Wetu, KINSHASA
  TIMU ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars” leo inafanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wa marudiano kutafuta tiketi ya kucheza Olimpiki 2020,Tokyo dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema leo kwamba kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu Bakari Shime 'Mchawi Mweusi' amesema wamekuja Congo kupambana na kupata ushindi.
  Shine amesema hakuna majeruhi katika kikosi hicho ambacho kiliwasili hapa Kinshasa jana mchana na jioni wakafanya mazoezi Uwanja wa shule ya Waturuki, Gombe, Kongo.

  Ameongeza kuwa mapungufu katika mchezo wa kwanza ameyafanyia kazi na wamekuja kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mchezo huo.
  Naye nahodha Asha Rashid amesema Wachezaji wamekuja kupambana kuhakikisha wanaiondosha DRC.
  Amesema kucheza ugenini hakuwapi tabu kwasababu mara kadhaa wameweza kuchukua ubingwa ugenini.
  Kikosi hicho kimetua na wachezaji 21 wote wakiwa katika hali nzuri na morali kubwa.
  Mchezo utachezwa saa 10 na nusu za jioni sawa na saa 12 na nusu kwa saa za Nyumbani Tanzania na utachezwa Stade des Martyrs
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS WAJINOA MARA YA MWISHO LEO KABLA YA KURUDIANA NA DRC KESHO KINSHASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top