• HABARI MPYA

  Wednesday, April 10, 2019

  ARSENAL NA CHELSEA KATIKA VITA MBILI TOFAUTI EUROPA LEAGUE

  BAADA ya kuangukia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Everton kwenye ligi wikendi iliyopiata, Arsenal wanatarajia kufanya vizuri Alhamisi hii watakapocheza kwenye Europa.
  ‘The Gunners’ wako nyumbani kukabiliana na Napoli kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali ya Europa League. Mechi hii ni muhimu sana kwa Arsenal hasa baada ya kupoteza mchezo wa wikendi.
  Arsenal kama ilivyo kwa Napoli wanaona Europa sio shindano la kiwango chao hivyo wanatamani kucheza kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya, ambayo Arsenal kwa misimu miwili iliyopita wameshindwa kufuzu kushiriki, na msimu huu pia bado wako kwenye hati hati ya kufuzu tena.
  Baada ya kufungwa na Everton walikuwa mbele ya Chelsea kwa tofauti ya magoli. Kila mtu kwenye klabu anajua kwamba wakishinda Europa basi moja kwa moja watashiriki ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao bila kujali wamemaliza katika nafasi gani kwenye msimamo wa ligi.
  Napoli wao watacheza michezo yote miwili bila kuwa na presha hiyo kwani wako katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Serie A. Mchezo huo utaonyeshwa LIVE kupitia ST World Football saa 4:00 Usiku kwenye StarTimes pekee.
  Beki na winga wa kulia wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles anasema, “Ni ndoto ya kila timu kucheza kwenye ligi ya Mabingwa, ndilo shindano kubwa zaidi la Ulaya duniani kote. Kucheza dhidi ya timu kubwa kunaleta nafasi nzuri ya kujipima”
  Upande mwingine Chelsea nao wanagombania vita mbili kama Arsenal.
  Wanacheza ugenini dhidi ya Slavia Prague kwenye mchezo wa kwanza ambao wanatarajiwa kushinda, wamekuwa kwenye kiwango kizuri katika shindano hili, wameshida michezo yote 10 na kuunga magoli ya kutosha, huku wakiongozwa na mfaransa Olivier Giroud ambaye amefunga mara tisa msimu huu.

  Japokuwa hawapewi nafasi sana, Slavia wameonyesha wana kila uwezo wa kufanya vizuri. Mzunguko uliopita waliwatoa wazoefu wa shindano hilo timu ya Sevilla hivyo Chelsea ni vyema wakawa makini. Mechi hii itakuwa LIVE saa 4:00 kupitia ST Sports Premium pekee.
  Michezo mingine ni kati ya Benfica na Eintracht Frankfurt, huku Valencia na Villarreal wanakutana katika mchezo wa wahispania pekee.
  Michezo ya marudiano itapigwa wiki ijayo Alhamisi.
  Wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi cha MAMBO kwa watumiaji wa Antenna na SMART kwa watumiaji wa Dish.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL NA CHELSEA KATIKA VITA MBILI TOFAUTI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top