• HABARI MPYA

  Monday, April 08, 2019

  SIMBA SC NA TP MAZEMBE KATIKA PICHA UWANJA WA TAIFA JUMAMOSI

  Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco 'Adebayor' (kulia) akitafuta maarifa ya kumpokonya mpira mchezaji wa TP Mazembe katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam timu hizo zikitoka sare ya 0-0.  
  Kiungo Mzambia wa Simba, Clatous Chama akipiga krosi pembeni ya beki wa TP Mazembe, Mganda Joseph Ochaya 
  Beki Mburkinabe wa Simba SC, Zana Coulibaly (kushoto) akimlamba chenga beki wa TP Mazembe, Kevin Mondeko Zatu 
  Kiungo Mnyarwanda wa Simba, Haruna Niyonzima akimiliki mpira katikati ya Uwanja pembeni ya beki wa TP Mazembe, Godet Masengo  
  Beki wa Simba, Serge Wawa Pascal (katikati) akimsabahi kipa wa TP Mazembe, Muivory Coast mwenzake, Sylvain Gbohouo 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed 'Mo' Dewji akizungumza na Rais wa klabu, Swedi Nkwabi
  Mashabiki wa Simba SC katika mchezo dhidi ya TP Mazembe Jumamosi Uwanja wa Taifa  
  Mashabiki wa Simba SC katika mchezo dhidi ya TP Mazembe Jumamosi Uwanja wa Taifa 
  Kikosi cha Simba SC kabla ya mchezo dhidi ya TP Mazembe Jumamosi Uwanja wa Taifa
  Kikosi cha TP Mazembe kabla ya mchezo dhidi ya Simba Jumamosi Uwanja wa Taifa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA TP MAZEMBE KATIKA PICHA UWANJA WA TAIFA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top