• HABARI MPYA

  Sunday, April 07, 2019

  SAMATTA ATOA PASI YA BAO LA PILI KRC GENK YAICHAPA GENT 2-1 LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana ametoa pasi ya bao la pili, KRC Genk ikiilaza 2-1 KAA Gent katika mchezo wa hatua ta pili ya Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Samatta alitoa pasi hiyo kwa kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy aliyefunga dakika ya 45 na ushei baada ya kufunga pia bao la kwanza dakika ya 43 kwa penalti, huku bao pekee la Gent likifungwa na Timothy Derijck dakika ya 87.
  Kwa ushindi huo wa pili ndani ya mechi tatu ikipoteza moja, Genk inaendelea kuongoza hatua ya pili ya Ligi ya Ubelgiji ijulikanayo kama Championship Round baada ya kuongoza pia hatua ya awali iitwayop Regular Season.
  Mbwana Samatta usiku wa jana ametoa pasi ya bao la pili, KRC Genk ikiilaza 2-1 KAA Gent

  Kwa Samatta mwenye umri wa miaka 26, jana amecheza mechi ya 149 kwenye mashindano yote na akiwa amefunga mabao 59 tangu amejiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 116 sasa na kufunga mabao 44 na kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili na Europa League amecheza mechi 24 na kufunga mabao 14.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Vukovic, Uronen, Lucumi, Dewaest, Maehle, Berge, Heynen, Malinovskyi, Trossard/Paintsil dk75, Ito na Samatta.
  KAA Ghent: Kaminski, Souquet, Verstraete, Sorloth, David/Limbombe dk75, Yaremchuk, Dejaegere/Chakvetadze dk75, Asare, Bronn, Esiti/Bezus dk62 na Derijck.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOA PASI YA BAO LA PILI KRC GENK YAICHAPA GENT 2-1 LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top