• HABARI MPYA

    Monday, April 08, 2019

    NAFASI YA TANZANIA RENKI ZA CAF BAADA YA MAFANIKIO YA SIMBA

    Na Hashim Mbaga, DAR ES SALAAM 
    HUKO nyuma tulishaelezana namna ya kupata point na kuweza kuwekwa rank kwa Nchi kulingana na mpangilio wa Timu shiriki na matokeo yake.
    Sasa tunataka kuangalia Tanzania ilipofika tunawezaje kunufaika na mfumo huu wa CAF ili tuweze kuingiza timu zaidi.

    HALI HALISI YA SASA
    Katika jedwali la mashindano ya 2020/2021 linaloonyesha nchi shiriki zinazotakiwa 12 za ziada, Tanzania ipo nafasi ya 12 ikiwa na point 18 na Kenya ipo nafasi ya 13 ikiwa na point 14.
    Nchi 10 zimeshaingia direct ila nafasi mbili zilizobaki zina nchi 3 nazo ni Tanzania 18, Kenya 14 na Angola 21.5 ila hii Angola haipo kwenye mashindano hivyo point zake zipo limit tayari inasubiri mmoja wetu atolewe hatua hii yeye aende direct.
    Katika matokeo yaliyokuwepo mpaka hivi sasa kwa Simba na pia Gor Mahia yakibaki kama yalivyo yaani tukatoka wote Tanzania inaingia direct kwenye nchi ya 12 hivyo kufanya kuweza kushiriki na kuingiza timu 2 Champion League na timu 2 Confederation Cup kwenye mashindano ya caf ya mwaka unaofuata yaani 2020/2021 yanayoanza October 2020. 

    UTAYARI BAADA YA KUPATA
    Tukishapata sasahivi hii nafasi ambayo tunaisubiria Simba inatuletea kama historia kwenye nchi yetu yatupasa ili tuweze kushiriki kila mwaka au mfululizo kuingiza timu 4 kwenye mashindano ya caf lazima tuwe na mkakati wa kitaifa katika kupata timu washindi washindani sio timu washindi washiriki nadhani mmeona mwaka huu Simba amekuwa Timu mshindi mshidani matokeo yake yameonekana.
    Kuanzia Bingwa wa ligi ya mwaka huu hii inayoendelea yaani bingwa wa TPL na FA lazima wawe ni timu zilizokamilika ili ziweze kupata Point za rank angalau sio chini ya 3 mpaka 4 ndio tunaweza kuendelea kushiriki tena.
    Maana Mabingwa wa Mwaka huu ushiriki wao caf interclub 2019/2020  point zake ndio zitatumika kwenye mashindano ya 2021/2022 wakati tayari kama Tanzania tutakuwa tumeshuka point toka 18 hadi 14 hivyo tukipata point kuanzia 3 tunakuwa rank ya point 29 kwenda mbele hapo ndio tunaweza kuendelea kuweka timu 4 lasivyo tutashiriki mwaka mmoja tu halafu basi tena na kupata hivyo point za rank hakuna mjadala ni lazima timu zingie group  Stage nje ya hapo hakuna kitu mbeleni tunaanza moja.
    Kutokana na mfumo ulivyo mashindano ya 2021/2022 Nchi 7 tu ndio zinakuwa limit kushiriki direct mpaka sasa kutokana na wingi wa point zao ila nafasi 5 zilizobaki nchi zote zinakuwa katika rank ya chini kuanzia point 25 kushuka chini Tanzania tukiwa na point 14 hivyo kufanya omgezeko la point ni juhudi za timu zenu shiriki kuingia group Stage ili uwezi kupata point zifike 29 kwenda mbele upate nafasi moja kati ya Tano zikizokuwepo.
    Kupanga ni kuchagua tukiamua tunaweza ila tukibaki kushangilia Azam FA fainali ya Dar City vs Lyon hatutafika mahali popote ni mfano tu.

    FAIDA YA KUSHIRIKI TIMU ZAIDI
    1. Heshima kwa nchi mwanachama.
    2. Inapunguza stress za kiuchumi na kisiasa katika jamii.
    3. Tunapata faida ya fedha kutokana na wingi wamichezo ya nyumbani, Mwaka huu Simba amefika hapa imecheza mechi hapa 6 sasa je tukiwa na timu 4 hatua za awali tu nyumbani mechi 8 ukiingiza timu mbili tu group Stage unauhakika wa mechi 6 nyumbani jumla 14 nyumbani.
    4. Vyanzo vya mapato kwa vilabu vyetu vinaongezeka na pia Ruzuku kwa TFF inaongezekavkufanya iweze kujiendesha.
    5. Kufanya soko la wachezaji wa kitanzania kukua maana mfano sasa simba imeweza kuonyesha vipaji vya wachezaji Watanzania zaidi ya 15 zikiwa timu zaidi unaongelea wachezaji 50 kuonekana Duniani na kupata EXPOSURE hata timu ya Taifa itakuwa nzuri  kutokana na hili.
    Kwa leo tuishie hapa mpaka hapo weekend tutakapopata matokeo ya Timu zetu za Gor Mahia na Simba kama Africa Mashariki.
    NI ZAMU YETU TANZANIA
    (Mwandishi wa makala hii, Hashim Mbaga anapatikana kwa namba +255 764 100 001)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAFASI YA TANZANIA RENKI ZA CAF BAADA YA MAFANIKIO YA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top