• HABARI MPYA

  Saturday, April 06, 2019

  MTIBWA SUGAR YAIPIGA ALLIANCE FC 1-0 MANUNGU, SINGIDA UNITED YAILAZA 2-1 KAGERA

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Alliance FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Ushindi huo uliotokana na bao pekee la Jaffary Salum Kibaya dakika ya 18, unaifanya Mtibwa Sugar inayofundishwa na kocha Zubery Katwila ifikishe pointi 45 baada ya kucheza mechi 31 na kupanda hadi nafasi ya tano kutoka ya sita.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Singida United imeshinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar mabao yake yakifungwa na Kenny Ally dakika ya kwanza kwa penalti na Himid Suleiman dakika ya 81 huku la wapinzani wao likifungwa na Omary Mponda dakika ya 11.

  Kwa ushindi huo, Singida United inafikisha pointi 39 baada ya kucheza mechi 32 na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 15.  
  Lipuli FC imelazimishwa sare ya 2-2 na Mwadui FC, mabao yake yakifungwa na Paul Nonga dakika ya 60 na Issa Rashid dakika ya 85, wakati ya timu ya Shinyanga yalifungwa na Wallace Kiango na Ditram Nchimbi dakika ya 70.
  Nayo JKT Tanzania imeshinda 1-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Meja Isamuhyo huku Tanzania Prisons ikilazimishwa sare ya 0-0 na Biashara United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAIPIGA ALLIANCE FC 1-0 MANUNGU, SINGIDA UNITED YAILAZA 2-1 KAGERA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top