• HABARI MPYA

  Sunday, April 07, 2019

  MSUVA APIGA BAO LA KWANZA DIFAA HASSAN EL – JADIDA YASHINDA 2-0 LIGI YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, CASABLANCA
  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku wa jana amefunga bao la kwanza, timu yake Difaa Hassan El –Jadida ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Rapide Oued Zem katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan.
  Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga aliyeibukia kwenye akademi ya Azam FC alifunga bao hilo dakika ya 40 baada ya kuwazidi mbinu walinzi wa Rapide Oued Zem. 
  Bao la pili la Difaa Hassan El –Jadida lilifungwa na mshambuiliaji mwingine tegemeo la timu hiyo, Bilal El Magri dakika ya 50.
  Simon Msuva akipongezwa na wenzake jana baada ya kufunga katika ushindi wa 2-0 wa Difaa Hassan El –Jadida dhidi ya Rapide Oued Zem

  Kwa matokeo hayo, Difaa Hassan El –Jadida inafikisha pointi 30 na kupanda hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa Botola Pro kutoka ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA APIGA BAO LA KWANZA DIFAA HASSAN EL – JADIDA YASHINDA 2-0 LIGI YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top