• HABARI MPYA

  Sunday, April 07, 2019

  HASSAN KESSY AISAIDIA NKANA FC KUIPIGA CS SFAXIEN 2-1 LEO KITWE KOMBE LA SHIRIKISHO

  BEKI Mtanzania, Hassan Ramadhani Kessy leo amesaidia klabu yake, Nkana FC kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya CS Sfaxien katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Nkana mjini Kitwe, Zambia.
  Sasa Nkana FC watakuwa na jukumu la kwenda kuulinda ushindi wao kwenye mchezo wa marudiano Jumapili ijayo Uwanja wa Taieb Mhiri mjini Sfax.
  Mabao ya Nkana FC leo yamefungwa na Kelvin Kampamba dakika ya 36 na Freddy Tshimenga dakika ya 52, wakati la CS Sfaxien lilifungwa na Habib Oueslati dakika ya 84.

  Hassan Kessy leo amesaidia Nkana FC kuichapa 2-1 CS Sfaxien ya Tunisia

  Kikosi cha Nkana FC kilikuwa; K. Malunga, J. Musonda, M. Mohammed, A. Bahn, Hassan Kessy, S. Malambo/J. Ngulube dk76, Duncan Otieno, K. Kampamba, F. Tshimenga/F. Mbewe dk71, R. Kampamba na W. Bwalya/S. Musonda dk62.
  CS Sfaxien; A. Dahmen, H. Mathlouthi, A. Zouaghi, H. Amamou, H. Dagdoug, N. Korichi/N. Zammouri dk72, H. Jelassi, K. Sokari, A. Harzi, H. Ben Ali/H. Oueslati dk56 na F. Chaouat.
  Mechi nyingine za Kombe la Shirikisho leo, Gor Mahia imefungwa 2-0 ntumbani Kenya na RSB Berkane ya Morocco, Etoile du Sahel imeshinda 3-1 dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan nchini Tunisia na mchezo kati ya wenyeji, Hassania Agadir na Zamalek ya Misri unaendelea hivi sasa Morocco timu hizo zikiwa hazijafungana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HASSAN KESSY AISAIDIA NKANA FC KUIPIGA CS SFAXIEN 2-1 LEO KITWE KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top