• HABARI MPYA

  Wednesday, April 10, 2019

  BENKI YA EXIM YAJITOSA SAFARI YA TAIFA STARS MISRI KWENYE AFCON YA 2019

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BENKI ya Exim leo imezindua kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri.
  Akizungumza wakati wa unzinduzi wa kampeni hiyo mjini Dar es Samaam leo, Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Andrew Lyimo alisema kampeni hiyo ya miezi miwili itakamilika mwanzoni mwa mwezi Junina ipo wazi kwa wateja wapya na wale ambao tayari wana akaunti za benki hiyo. 

  “Kampeni hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa mkakatiwa benki ya Exim katika kusimamia ustawi wa wateja unaofahamika kama 'Exim kazini leo, kwa ajili ya kesho' (Exim at Work Today, for tomorrow) unaoendana na dira na muelekeo wa benki hiyo. Ni kampeni inayothibitisha nia ya benki ya Exim katika kutafuta kesho iliyo bora kwawateja na jamii inayoizunguka.’’ Alisema.
  Alisema washindi wa kampeni hiyo watapata fursa ya pekee ya kufurahia mchezo wanaoupenda huku pia wakipata fursa ya kuungana na Taifa Stars katika mashindano hayo huku wakiwa wamelipiwa gharamazote za safari ikiwemo gharaza na Visa, tiketi ya ndege,gharamza za tiketi ya kushuhudia mechi hizo pamoja na fedha za kujikimu. "Jumla kutakuwa na washindi watano ambapo washindi wawili watapatikana katika mwezi wa awali wa kampeni na washindi wa wengine watatu watapatikana katika mwezi wa mwisho wa kampeni hii.’’ Alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENKI YA EXIM YAJITOSA SAFARI YA TAIFA STARS MISRI KWENYE AFCON YA 2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top