• HABARI MPYA

  Saturday, April 06, 2019

  MAMELODI YAIPIGA AL AHLY 5-0 ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

  TIMU ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imetanguliza mguu mmoja Nusu Fainali ya Ligi Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri leo Uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe mjini Pretoria.
  Sasa Mamelodi Sundowns inayofundishwa na kocha mzalendo, Pitso John Mosimane itakuwa na kazi nyepesi ya kuulinda ushindi wake mnene kwenye mchezo wa marudiano wa Robo Fainali  Aprili 13 mjini Alexandria.
  Mabao ya Mamelodi leo yamefungwa na Themba Zwane dakika ya 14, Wayne Arendse dakika ya 24, Ricardo Nascimento kwa penalti dakika ya 47, Leandro Gastón Sirino dakika ya 62 na Phakamani Mahlambi dakika ya 83.

  Mechi za kwanza za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo, Simba SC imelazimishwa sare ya 0-0 na Tout Puissant Mazembe Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Simba SC watajilaumu wenyewe kwa sare hiyo ya nyumbani, kwani walipoteza nafasi nzuri mno ya kuibuka na ushindi kipindi cha pili, kufuatia Nahodha wake, John Raphael Bocco kukosa penalti.
  Mchezo kati ya Horoya ya Guinea na Wydad Casablanca unaendelea hivi sasa na baadaye CS Constantine ya Algeria itamenyana na Esperance Uwanja kuanzia Saa 4:00 usiku. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMELODI YAIPIGA AL AHLY 5-0 ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top