• HABARI MPYA

  Wednesday, March 06, 2019

  YANGA SC WAIFUATA TENA ALLIANCE FC MJINI MWANZA KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itasafiri kuifuata tena Alliance FC mjini Mwanza katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mwishoni mwa mwezi huu.
  Hiyo ni baada ya droo ya hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo iliyopangwa leo makao makuu ya Azam TV, wadhamini wa michuano hiyo, Tabata mjini Dar es Salaam.
  Katika droo hiyo, vigogo wengine, Azam FC nao watasafiri kwenda Kanda ya Ziwa, mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar.

  Robo Fainali nyingine, KMC watamenyana na African Lyon Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam na Lipuli FC dhidi ya Singida Uwanja wa Samora mjini Iringa.  
  Iwapo itafanikiwa kuingia Nusu Fainali, Yanga itaendelea kucheza ugenini kwani itakutana na mshindi kati ya Lipuli FC na Singida United, aidha Uwanja wa Samora au Namfua.
  Mshindi wa mchezo kati ya Kagera Sugar na Azam FC atamenyana na mshindi wa mchezo kati ya KMC na African Lyon katika Nusu Fainali nyingine mwishoni mwa mwezi Apirli na Fainali itafanyika mwezi Juni Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAIFUATA TENA ALLIANCE FC MJINI MWANZA KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top