• HABARI MPYA

  Wednesday, March 06, 2019

  SERENGETI BOYS YAFUFUA MAKALI ULAYA, YAICHAPA AUSTRALIA 3-2 MICHUANO YA UEFA ASSIST

  Na Mwandishi Wetu, ANTALYA
  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imepata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya UEFA Assist U-17 baada ya kuichapa Australia mabao 3-2 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Emirhan Sports Complex mjini Antalya nchin Uturuki.
  Mabao ya Serengeti Boys katika mchezo wa leo yamefungwa na mshambuliaji wake hatari, Kelvin John mawili dakika za 16 na 84 na Edson Mshirakandi dakika ya 87.
  Na hiyo ni baada ya Australia kumaliza kipindi cha kwanza ikiwa inaongoza 2-1, mabao yake yakifungwa na Michael Ruhs dakika ya 13 na Noah Boatic dakika ya 45.

  Mechi za kwanza Serengeti Boys ilichapwa 1-0 na Guinea, wakati Australia ilifungwa 4-1 na wenyeji Uturuki. Serengeti Boys itakamilisha mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na Uturuki, huku Australia ikimenyana na Guinea.
  Wakati Kundi A linaundwa na Tanzania, Guinea, Australia na wenyeji, Uturuki, Kundi B linazikutanisha Cameroon, Uganda, Morocco na Belarus na Kundi C lina timu za Senegal, Nigeria, Angola na Montenegro. 
  Tanzania inatumia michuano hiyo kama maandalizi yake ya mwisho ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) ambayo wao watakuwa wenyeji kuanzia Aprili 14 hadi 28 mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAFUFUA MAKALI ULAYA, YAICHAPA AUSTRALIA 3-2 MICHUANO YA UEFA ASSIST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top