• HABARI MPYA

    Monday, March 04, 2019

    SERENGETI BOYS YAANZA VIBAYA MICHUANO YA UEFA ASSIST, YACHAPWA 1-0 NA GUINEA

    Na Mwandishi Wetu, ANTALYA
    TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeanza vibaya michuano ya UEFA Assist U-17 baada ya kuchapwa 1-0 na Guinea katika mchezo uliofanyika mjini Antalya, Uturuki leo.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Emirhan Sports Complex mjini Antalya nchin Uturuki, bao pekee la Guinea lililoizamisha Tanzania inayofundishwa na Kocha Oscar Milambo limefungwa na mshambuliaji Abubakar Konte dakika ya 26.
    Mechi hiyo ilichezwa kwenye baridi huku barafu zikidondoka, hali ambayo dhahiri ilionekana kuwaathiri wachezaji wa Tanzania. 
    Mshambuliaji Kelvin John wa Serengeti Boys akipambana na wachezaji wa Guinealeo mjini Antalya 
    Wachezaji wa Tanzania na Guinea wakiwania mpira wa juu leo mjini Antalya
      
    Tanzania imepangwa Kundi A pamoja na Guinea, Australia na wenyeji, Uturuki, wakati Kundi B linaundwa na timu za Cameroon, Uganda, Morocco na Belarus na Kundi C lina timu za Senegal, Nigeria, Angola na Montenegro. 
    Tanzania inatumia michuano hiyo kama maandalizi yake ya mwisho ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) ambayo wao watakuwa wenyeji kuanzia Aprili 14 hadi 28 mjini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAANZA VIBAYA MICHUANO YA UEFA ASSIST, YACHAPWA 1-0 NA GUINEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top