• HABARI MPYA

  Wednesday, March 06, 2019

  AJAX YAIVUA UBINGWA REAL MADRID BAADA YA KUICHAPA 4-1 BERNABEU

  David Neres akipiga shuti kumtungua kipa Thibaut Courtois kuifungia bao la pili Ajax dakika ya 18 baada ya kupokea pasi ya Dusan Tadic katika ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Real Madrid usiku wa jana kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Bernabeu. Mabao mengine ya Ajax yamefungwa na Hakim Ziyech dakika ya saba, Dusan Tadic dakika ya 62 na Lasse Schone dakika ya 72, wakati la Real Madrid limefungwa na Marco Asensio dakika ya 70.
  Kwa matokeo hayo, Ajax inasonga mbele kwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-3 kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Amsterdam 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AJAX YAIVUA UBINGWA REAL MADRID BAADA YA KUICHAPA 4-1 BERNABEU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top