• HABARI MPYA

  Saturday, March 09, 2019

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA STAND UNITED 2-0, AFRICAN LYON YAPIGWA NYUMBANI NA PRISONS

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  TIMU ya Mtibwa Sugar imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani, Manungu uliopo Turiani mkoani Morogoro kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United ya Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo.
  Mabao yaliyoipa ushindi huo Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Riphat Khamis dakika ya 46 na Haruna Chanongo dakika ya 89.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi 27 na kupanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakati Stand United inayobaki na pointi zake 33 za mechi 30 sasa, inateremka kwa nafasiu moja hadi ya 16.

  Mechi nyingine za leo, Tanzania Prisons imeendelea kufanya vyema chini ya kocha mpya, Mohammed Rishard ‘Adolph’ baada ya kuwachapa wenyeji, African Lyon mabao 2-1 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Mabao yote ya Prisons yamefungwa na Adam Adam dakika ya 51 ba 69, wakati la African Lyon limefungwa na Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dakika ya 13.
  Prisons sasa inafikisha pointi 35 baada ya kucheza mechi 29 na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 17, wakati Lyon inabaki nafasi ya mwisho, 20 na pointi zake 22 za mechi 30 sasa.
  Kagera Sugar imekubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa Coastal Union bao pekee la Raizin Hafidh dakika ya 20 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Coastal Union inafikisha pointi 37 baada ya ushindi huo katika mechi ya 29 na kupanda hadi nafasi ya saba, wakati Kagera Sugar inashuka kwa nafasi moja hadi ya 14 ikibaki na pointi zake 33 za mechi 28 sasa.
  Na bao pekee la Jimmy Shoji dakika ya 35 limetosha kuipa ushindi wa 1-0 Lipuli FC dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Kwa ushindi huo, Lipuli ya kocha Suleiman Matola inafikisha pointi 41 katika mechi ya 30, ingawa inabaki nafasi ya tano wakati Mbao ya Mwanza inayobaki na pointi zake 36 baada ya kucheza mechi 29 sasa inateremka kwa nafasi mbili hadi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA STAND UNITED 2-0, AFRICAN LYON YAPIGWA NYUMBANI NA PRISONS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top