• HABARI MPYA

  Tuesday, March 05, 2019

  MCHEZAJI AFARIKI UWANJANI AKIICHEZEA TIMU YAKE GABON

  MSHAMBULIAJI Herman Tsinga alifariki dunia Jumamosi wakati akiichezea klabu yake,  Akanda FC katika Ligi Daraja la Kwanza Gabon mjini Libreville.
  Taarifa za za vyombo vya Habari zimesema kwamba Tsinga, tegemeo la Akanda FC, alizimia dakika ya 23 wakati wa mchezo dhidi ya Missile FC, gazeti la kila siku la Union limeripoti.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ilielezwa alipatwa tatizo la moyo kwa mujibu wa Daktari wa Jeshi, lakini akafariki akiwa njiani anakimbizwa hospitali.

  Video ya kiwango cha chini iliyopostiwa Twitter inaonyesha mkanganyiko wa hatua zilizochukuliwa baada ya Tsinga  karibu na katikati ya Uwanja.
  Kwa mujibu wa gazeti la Union, hakuna kati ya ambulances mbili zilizokuwepo kwenye eneo la tukio lilikuwa na kifaa cha oxygen ili kuokoa maisha ya mchezaji huyo.
  Hicho kinakuwa kifo cha saba ndani ya miaka 12 kwenye soka ya Gabon kwa mujibu wa gazeti la Union.
  Mechi hiyo ilikuwa ni sehemu ya mzunguko wa pili wa ligi, ambao ulianza Februari kufuatia kuchelewa kwa miezi nane hadi kampuni ya Mafuta Gabon ilipokubali kudhamini michuano hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI AFARIKI UWANJANI AKIICHEZEA TIMU YAKE GABON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top