• HABARI MPYA

  Thursday, March 07, 2019

  MAN UTD YAIPIGA PSG 3-1, YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

  Mshambuliaji wa kimataifa wa England, Marcus Rashford (katikati) akishangilia kishujaa baada ya kuifungia Manchester United bao la tatu dakika ya 90 na ushei kwa penalti kufuatia Presnel Kimpembe kuunawa mpira katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Paris Saint-Germain usiku wa jana Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Ufaransa. Mabao mengine yalifungwa na mshambuliaji Mbelgiji Romelu Lukaku dakika ya pili na 30, wakati la PSG lilifungwa na beki Mspaniola, Juan Bernat dakika ya 12 na kwa matokeo hayo Manchester United inakwenda Robo Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3 kufuatia kufungwa 2-0 nyumbani kwenye mchezo wa kwanza mwezi uliopita 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UTD YAIPIGA PSG 3-1, YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top