• HABARI MPYA

  Friday, March 08, 2019

  ARSENAL PUNGUFU YAGONGWA 3-1 UFARANSA EUROPA LEAGUE

  Refa Ivan Kruzliak akimuonyesha kadi nyekundu beki Mgiriki wa Arsenal, Sokratis Papastathopoulos dakika ya 41 kufuatia kumuonyesha kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu  Ismaila Sarr wa Rennes katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Roazhon Park mjini Rennes, Ufaransa. Renees ilishinda 3-1, mabao yake yakifungwa na Benjamin Bourigeaud dakika ya 42, Nacho Monreal aliyejifunga dakika ya 65 na Sarr dakika ya 88, wakati la Arsenal inayotakiwa kushinda 2-0 kwenye mchezo wa marudiano Machi 14 London, lilifungwa na Alex Iwobi dakika ya tatu 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL PUNGUFU YAGONGWA 3-1 UFARANSA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top